Rais Vladmir Putin wa Russia ameituhumu Washington kuwa inatoa
msaada wa kilojistiki wa moja kwa moja kwa wanamgambo wa Qafqazi ya
Kaskazini. Putin amesema Jumapili hii katika televisheni ya Rossiya 1
kuwa, vyombo vya kiitelijinsia vya Russia vimepata ushahidi unaoashiria
msaada uliokuwa ukitolewa na Marekani kwa wanamgambo wa Qafqazi ya
Kaskazini mwanzoni mwa mwaka 2000. Rais Vladmir Putin wa Russia
amebainisha hayo Jumapili hii katika filamu iliyopewa jina la "Rais" kwa
mnasaba wa kuadhimisha miaka 15 tangu awe Rais wa nchi kwa mara ya
kwanza. Rais Putin amesema alimtaarifu Rais wa Marekani wa wakati huo
kuhusu hatua za uingiliaji kati za Washington, na kisha Rais wa Marekani
alimjibu kwa kusema, atasitisha misaada ya nchi yake kwa waasi hao wa
Qafqazi ya Kaskazini. Hata hivyo baada ya siku 10, wakuu wa shirika la
ujasusi la Russia FSB walipokea barua kutoka kwa wenzao wa Washington
wakisema kuwa, wamekuwa na wataendelea kuwa na mahusiano na makundi ya
upinzani ya Russia; na kwamba wanaona wana haki ya kufanya hivyo, na
wataendelea kufanya hivyo hata katika siku za usoni.
No comments:
Post a Comment