Watu wasioungua watatu wamejeruhiwa katika mripuko wa bomu la
kutegwa kwenye gari uliotokea leo katika kitongoji cha Givatayim huko
Tel Aviv. Mripuko huo wa bomu umewajeruhi watu watatu huku mmoja akiwa
na hali mbaya. Mripuko huo wa bomu la kutegwa garini umetokea leo huko
Tel Aviv, siku moja baada ya maafisa wanne wa polisi wa Israel
kujeruhiwa kwa kugongwa na gari katika mji wa Quds. Matukio hayo yote
yamejiri huku hali ya wasiwasi ikitanda kufuatia kuuliwa kijana wa
Kipalestina katika kivuko cha upekuzi cha jeshi la Israel katika mji wa
Quds. Wapalestina kadhaa walijeruhiwa pia katika ghasia zilizotokea kati
yao na wanajeshi wa Israel huko Quds Mashariki.
Ripoti zimeeleza kuwa, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel juzi usiku walimfyatulia risasi kijana wa Kipalestina aliyekuwa na umri wa miaka 16 wakati alipokuwa akielekea katika kituo hicho cha upekuzi akiwa pamoja na familia yake. Wanajeshi wa Israel walidai kuwa Mpalestina huyo eti alikusudia kumdhuru afisa wa Israel.

No comments:
Post a Comment