Maelfu ya wakazi wa mashariki mwa Saudi Arabia wameandamana
wakipinga mashambulizi ya kijeshi yanayoendelea kufanywa na jeshi la
nchi hiyo dhidi ya watu wa Yemen.
Maandamano hayo yaliyofanyika jana jioni katika mji wa Awwamiya yamekosoa mashambulizi ya Saudia dhidi watu wa Yemen na kutoa nara dhidi ya utawala wa kifalme wa nchi hiyo. Washiriki katika maandamano hayo vilevile walikuwa na mabango ya picha za Sheikh Nimr Baqir al Nimr, mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu wa Saudi Arabia anayeshikiliwa katika korokoro za nchi hiyo. Waandamanaji hao wametaka kuachiwa huru msomi huyo wa Kiislamu anashikiliwa kutokana na kupigania haki za kimsingi za Waislamu wa madheheu ya Shia nchini Saudi Arabia.
Maeneo ya mashariki mwa Saudia hususan mji wa Qataf ambayo yana idadi kubwa zaidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, yamekuwa yakishuhudia maandamano ya mara kwa mara kupinga dhulma na ukandamizaji wa utawala wa kifalme nchi hiyo. Makumi ya raia wa maeneo hayo wameuawa kwa kupiga risasi na polisi na wengine wengi wanashikiliwa katika korokoro za nchi hiyo

No comments:
Post a Comment