Mawaziri wa Ulinzi wa nchi kadhaa za
Afrika Mashariki wanakutana Khartoum mji mkuu wa Sudan katika mkutano
wa siku tatu wenye lengo la kujadili changamoto za kiusalama. Mawaziri
wa Ulinzi wa Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Visiwa
vya Comoro, Sudan Kusini, Ushelisheli na mwenyeji Sudan wanashiriki
katika mkutano huo ulioanza jana. Akihutubia katika kikao cha ufunguzi
wa mkutano huo, Abdul Rahim Muhammad Hussein, Waziri wa Ulinzi wa Sudan
amesema kuwa, ni jambo la dharura kwa nchi za Afrika Mashariki kufanya
kila ziwezalo kukabiliana na changamoto za kiusalama zinazozikabili.
Amesema kuwa, kuna haja ya kutumiwa suhula na mikakati yote kwa ajili ya
kukabiliana na migogoro ili kuhakikisha amani na uthabiti vinatawala
barani Afrika. Aidha Waziri wa Ulinzi wa Sudan amesisitiza juu ya kuweko
uratibu wa juhudi kwa lengo la kuhitimisha migogoro, mivutano na
mapigano sambamba na kupunguza machungu ya watu kupitia ufumbuzi wa
kisiasa, kiusalama na ustawi wa mwanadamu. Waziri wa Ulinzi wa Sudan
ametoa wito pia wa kuimarishwa sekta ya ulinzi kwa nchi za Kiafrika kwa
kutumiwa vyema vyanzo vya utajiri na uwezo wa nguvu kazi ya bara la
Afrika
No comments:
Post a Comment