Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran
SEPAH, Mohammad Ali Jafari amesema kuwa, mashambulizi ya utawala wa
Saudi Arabia nchini Yemen yameuweka utawala huo mahala ulipofikia
utawala wa Kizayuni wa Israel na kusisitiza kuwa, uongozi wa Aal Saud
unaelekea kuanguka na kusambaratika kabisa.
Kamanda Jafar ameyasema hayo leo katika tamasha ya sita ya elimu ya tiba ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliyopewa jina la 'Baqirul-Ulum' na kuongeza kuwa, mashambulizi hayo ya Saudia yamevuka mipaka yote ya Kiislamu kwa kuwa yanatekelezwa dhidi ya nchi ya Waislamu ambayo inafanya juhudi za kuwa huru. Amesisitiza kuwa, hatua ya utawala wa Aal Saudi kuwasaliti Waislamu kwa kutekeleza matakwa ya utawala wa Kizayuni, itaufanya usambaratike hivi karibuni. Kamanda wa jeshi la SEPAH amesema kuwa, umefika wakati wa kutouonea tena haya utawala huo kwa maovu yake nchini Yemen dhidi ya watu wasio na ulinzi.
Meli na ndege za kivita za Saudia zimeendeleza mashambulizi kwa wiki ya nne sasa nchini Yemen kuua idadi kubwa ya watu na wengine wengi kujeruhiwa. Leo ndege hizo zimeshambulia kambi ya jeshi mjini Sana'a sanjari na kuyalenga maeneo tofauti ya nchi hiyo yakiwemo makazi ya raia.

No comments:
Post a Comment