Mawaziri wa Ulinzi wa Iran na Syria wamesisitiza juu ya udharura wa kudumishwa mapambano ya pande zote dhidi ya ugaidi.
Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Hussein Dehqan amesema
vita vya kulazimishwa vya matakfiri na Uzayuni dhidi ya wananchi wa
Syria ni vita vinavyopiganwa kwa niaba ya upande mwingine na stratejia
ya pamoja ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel. Brigedia
Jenerali Dehqan amesema kuwa lengo la vita hivyo ni kuudhaminia usalama
wa kudumu utawala wa Kizayuni, kuzidhoofisha na kuzigawa nchi za
Kiislamu, kubadili muundo wa eneo la Mashariki ya Kati, kukabiliana na
wimbi la mwamko wa Kiislamu na mwishowe kulidhibiti kikamilifu eneo la
Mashariki ya Kati.
Waziri wa Ulinzi wa Iran ameyasema hayo leo hapa Tehran katika
mazungumzo yake na Fahd Jasim al Furayj, Waziri wa Ulinzi wa Syria
aliyeko ziarani nchini Iran.
Brigedia Jenerali Hussein Dehqan amepongeza muqawama na mapambano ya
wananchi na vikosi shupavu vya jeshi la Syria dhidi ya magaidi na
vibaraka kutoka nchi mbalimbali duniani na kuongeza kuwa: Kuendelezwa
muqawama huo kusambaratishaa makundi ya kitakfiri na kigaidi.
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi wa Syria Meja Jenerali Fahd Jassem
al-Freij amewapongeza wananchi na serikali ya Iran kwa kuwaunga mkono
wananchi na serikali ya Syria katika mapambano yao dhidi ya magaidi na
kueleza kuwa: Wananchi wa Syria kamwe hawatasahau msaada na uungaji
mkono wa wananchi na serikali ya Iran. Waziri wa Ulinzi wa Syria amesema
kuwa Iran ya Kiislamu ni mhimili na msingi mkuu wa mapambano na
kuongeza kuwa, ushindi huu mkubwa usingepatikana iwapo kusingekuwepo
uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
No comments:
Post a Comment