Tuesday, 28 April 2015
Maelfu waandamana Yemen kulaani ukatili wa Saudia
Huku ndege za kivita za utawala wa Aal Saudi zikiendeleza mashambulizi yake ya kichokozi nchini Yemen, leo maelfu ya raia wa nchi hiyo wamemiminika mabarabarani mjini Sana'a wakilaani mwendelezo wa hujuma hiyo ya Saudia. Maandamano hayo yaliyowashirikisha viongozi wa asasi mbalimbali nchini Yemen, yamepewa anwani ya 'Tuko Pamoja Kupinga Uadui wa Saudia na Marekani.' Viongozi mbalimbali wametoa hotuba kali dhidi ya utawala wa Aal- Saud na kusisitiza kuwa, Wayemen pekee ndio watakaainisha mustakbali wa taifa lao kinyume na mashinikizo ya Riyadh. Waandamanaji hao pia wamepinga aina yoyote ya mazungumzo au mapatano na Saudia chini ya anga ya mashambulizi.
Hayo yanajiri huku idadi ya wahanga waliouawa kutokana na mashambulizi hayo ikipindukia 3512 na zaidi ya wengine 6000 kujeruhiwa. Kwa mujibu wa Taasisi ya Kutetea Haki za Binaadamu nchini Yemen, watoto 492 na wanawake 209, ni miongoni mwa watu waliouawa katika mashambulizi hayo ya kikatili ya Saudia na waitifaki wake. Ripoti hiyo imesema maelfu ya nyumba za raia pia zimeharibiwa katika mashambulizi ya kinyama ya Suadi Arabia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment