Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu
za rambirambi kwa Rais wa Nepal kutokana na maafa yaliyosababishwa na
mtetemeko wa ardhi uliotokea jana nchini humo na kuua karibu watu elfu
mbili.
Ujumbe wa Rais Rouhani kwa mwenzake wa Nepal, Ram Baran Yadav umesema
Iran imesikitishwa na kuhuzunishwa sana na habari ya tetemeko la ardhi
na vifo vya idadi kubwa ya watu wa Nepal. Rais Rouhani ameongeza kuwa,
sambamba na kutoa salamu za rambirambi kwa rais, taifa la Nepal pamoja
na ndugu wa wahanga wa tetemeko hilo, anawatakia ahueni waliojeruhiwa na
kuwaombea dua njema.
Ripoti za hivi karibuni zinasema kuwa mtetemeko mkubwa wa ardhi
uliotokea jana karibu na mji mkuu wa Nepal, Kathmandu umeua watu
wasiopungua 1900.
Wakati huo huo Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran imetangaza kuwa iko tayari kutuma misaada ya dharura kwa watu
walioathiriwa na mtetemeko wa jana nchini Nepal
No comments:
Post a Comment