Mamilioni ya wananchi wa Benin leo wameeleka kwenye masanduku ya
kupigia kura kuwachagua wawakilishi wao katika bunge la nchi hiyo.
Kamisheni ya Uchaguzi ya Benin imetangaza kuwa Wabenin karibu milioni
4 wametimiza masharti ya kupiga kura na kwamba wabunge 83 watachaguliwa
moja kwa moja katika uchaguzi wa leo.
Umoja wa Afrika (AU) umetuma maafisa 40 kwa ajili ya kusimamia zoezi
hilo la uchaguzi, kuhesabiwa kura na utangazaji wa matokeo yake. Ujumbe
huo unaongozwa na rais wa zamani wa Mali.
Uchaguzi wa Bunge nchini Benin unafanyika siku chache tu baada ya
chaguzi za rais zilizofanyika kwa amani na utulivu katika nchi za Togo
na Nigeria, jambo ambalo limetajwa kuwa ni ishara ya kuimarika
demokrasia barani Afrika
No comments:
Post a Comment