Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch
limetangaza kuwa Waislamu wasiopungua 42 wengi wao wakiwa wanawake na
wasichana, wanaoshikiliwa mateka na kundi la wanamgambo wa Kikristo la
Anti-Balaka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) wanakabiliwa na
hatari ya kunajisiwa.
Taarifa iliyotolewa jana na HRW imewataka askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na maafisa wa serikali ya ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kuingilia haraka na kukomboa kundi hilo la wafugaji Waislamu wa kabila la Fulani wanaoshikiliwa mateka tangu mwaka mmoja uliopita.
Taarifa ya Human Rights Watch imesema kuwashikilia raia kama mateka, kuua watoto na kuwafanya wanawake na wasichana kuwa watumwa wa ngono ni mbinu za kutisha zinazotumiwa na Anti-Balaka na yote hayo ni jinai za kivita.
Taarifa hiyo imetolewa siku tatu baada ya kuokolewa wafugaji 21 Waislamu wakiwemo wanawake 6 na watoto 13 kutoka mikononi mwa wanamgambo wa Anti-Balaka. Ripoti ya HRW imesema wanawake 3 kati yao wamenajisiwa na wako katika hali mbaya.
Maelfu ya Waislamu wameuawa na wengine milioni moja kulazimika kukimbia makazi yao baada ya kundi la Kikristo la Anti-Balaka kuanzisha mashambulizi dhidi ya mahasimu wao wa Seleka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati hapo mwaka 2013.

No comments:
Post a Comment