Mwanafunzi wa chuo kikuu nchini Marekani amemlaumu vikali mgombea
tarajiwa wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Republican Jeb Bush
na kumfahamisha bayana kuwa kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) liliundwa
na kaka yake, rais wa zamani wa Marekani George W. Bush.
Tukio hilo limejiri katika mkutano wa kampeni katika jimbo la Nevada
siku ya Jumamosi baada ya Jeb Bush kumaliza mkutano huo. Jeb Bush
aliwahi kuwa Gavana wa Florida na anatazamiwa kutangaza azma yake ya
kuwania urais katika uchaguzi ujao wa rais mwaka 2016.
Ivy Ziedrich, mwanaharakati wa kisiasa, alimbana vikali Jeb kuhusu
hatua ya George W Bush kuvamia Iraq na hatimaye kuunda kundi la kigaidi
la ISIS. Mwanaharakati huyo amemfahamisha Jeb Bush kuwa kaka yake
alivamia Iraq na kuwaachia kwa makusudi wanamgambo wapate silaha za
kisasa.
Jeb Bush alipinga kauli hiyo, hata hivyo alisema kuna baadhi ya
makosa yaliyofanywa na rais wa wakati huo wa Marekani katika kutuma
majeshi nchini Iraq.
No comments:
Post a Comment