Hali ya wasiwasi imezidi kutanda katika mkoa wa mashariki mwa
Saudi Arabia siku mbili baada ya kutokea shambulio la bomu katika
Msikiti wa Imam Ali AS huko al Qadeeh.
Leo wakazi wa mji wa al Qadeeh wamefanya maandamano makubwa wakilalamikia serikali ya Saudia kwa kushindwa kuwalinda.
Waandamanaji wamewaambia waandishi wa habari kuwa vikosi vya usalama vya Saudi Arabia vimewatelekeza wakazi wa mji huo na kutoa mwanya wa makundi ya kigaidi kama Daesh kufanya mashambulizi hadi misikitini.
Wakati huo huo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia imesema kuwa, aliyefanya shambulio la kigaidi la siku ya Ijumaa katika Msikiti wa Imam Ali AS huko al Qadeeh ni raia wa Saudia anayejulikana kwa jina la Salih bin Abdulrahman Salih al Ghisaami.
Wizara hiyo imeongeza kuwa, gaidi huyo alikuwa anasakwa na maafisa usalama wa Saudia kwa kuwa na mfungamano na kundi la kitakfiri la Daesh ambalo hadi sasa limeshaua maelfu ya watu katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu wa Kiarabu.

No comments:
Post a Comment