Watu wasiopungua 19 wameuawa katika mapigano yaliyozuka baina ya
waasi wa Tuareg na wanajeshi wa serikali, kaskazini mwa Mali. Wizara ya
Ulinzi ya Mali imetoa taarifa ikisema kuwa, wanajeshi 9 wameuawa baada
ya waasi wa Tuareg wa CMA wanaopigania kujitenga eneo la Azawad
kuushambulia mji wa Lere karibu na mpaka wa Mali na Mouritania siku ya
Jumatano. Taarifa hiyo ya jana ya Wizara ya Ulinzi ya Mali imeongeza
kuwa, wanajeshi wengine 6 wamejeruhiwa kwenye shambulio hilo na wengine
sita kutekwa nyara. Wanajeshi wa Mali walifanikiwa kuua waasi 10 wa
Tuareg na kuwajeruhiwa wengine 16 kwenye mapigano hayo. Vile vile
walifanikiwa kuharibu magari ya waasi hao na kuteka silaha zao kadhaa.
Wakati huo huo Waziri wa Ulinzi wa Mali Tieman Hubert Coulibaly amesema
kuwa mji wa Mali bado umo mikononi wa serikali. Eneo la kaskazini mwa
Mali limeshuhudia siku kadhaa za machafuko. Serikali ya Bamako
inawalaumu waasi kwa kuchoche machafuko hayo ikisema kuwa waasi hao
wamekusudia kuharibu kwa makusudi mwenendo wa mazungumzo ya amani nchini
humo.
No comments:
Post a Comment