Habari kutoka mji wa Beni, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo zinasema kuwa watu wasiopungua 20 wameuawa katika mazingira ya
kutatanisha katika kipindi cha siku tatu zilizopita. Mashuhuda
wameiambia idhaa hii kwamba maiti za watu 20 zilizokatwa vipande vipande
zimetapakaa katika vichaka na misitu ya karibu na mji wa Beni na kwamba
serikali imesisitiza kuwa waasi wa kutoka Uganda wa ADF-Nalu ndio
waliotekeleza mauaji hayo. Hii ni katika hali ambayo, jeshi la DRC miezi
miwili iliyopita lilitangaza kuwa limeharibu ngome nyingi za waasi hao
katika maeneo mengi hususan katika mikoa ya Kivu Kusini na Kaskazini
inayopatikana mashariki mwa nchi hiyo.
Eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limekuwa
likikumbwa na mauaji yanayotokana na hujuma za makundi ya waasi; na
wafuatiliaji wengi wa mgogoro wa nchi hiyo wanasema waasi hupiga kambi
mashariki mwa DRC kutokana na eneo hilo kuwa na rasilimali nyingi kama
vile madini yenye thaman
No comments:
Post a Comment