Monday, 11 May 2015
Afkham: Madai ya Ahmad Shaheed ni urongo mtupu
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran amesema kuwa, madai ya Ahmad Shaheed, Ripota Maalumu wa Baraza la
Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Iran
kwamba, hapa nchini kumekuwa kukitekelezwa unyongaji wa watu kwa siri na
kunyongwa pia wafungwa wa kisiasa ni urongo mtupu. Marzieh Afkham
amebainisha kwamba, madai hayo yanakinzana wazi na majukumu yake. Afkham
amesema, Iran imebainisha mara chungu nzima kwamba, Ahmad Shaheed
amekuwa akitegemea vyanzo vya uongo katika kuandaa ripoti zake ambazo
zinapingana na uhalisia wa mambo. Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya
Kigeni ya Iran amebainisha kwamba, inasikitisha mno kwamba, utendaji
kazi wa Ripota Maalumu wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa
anayeshughulikia Masuala ya Iran hauko katika mkondo sahihi na
hautegemei ushahidi wa kweli. Amesema, madai hayo ya mara kwa mara dhidi
ya Iran yana malengo ya kisiasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment