Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa,
inabidi mji wa Khorramshahr (wa kusini magharibi mwa Iran) wenye utajiri
wa mafuta ukombolewe kutoka katika mashinikizo ya kundi la 5+1 na
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Rais Rouhani amesema hayo leo katika maadhimisho ya siku ya ukombozi wa mji wa Khorramshahr na kuongeza kuwa, ardhi ya kiuchumi ya Iran imetekwa na Baraza la Usalama na kundi la 5+1 na kusisitiza kuwa, kama ambavyo makamanda wa kijeshi wa Iran walifanikiwa kuukomboa mji wa Khorramshahr kutoka mikononi mwa wanajeshi vamizi wa Iraq, viongozi wa kisiasa nao wataikomboa Khorramshahr mpya kutoka kwenye mashinikizo ya madola ya kigeni.
Amesema, Iran ni taifa ambalo haliwezi kamwe kuusahau ukombozi wa Khorramshahr na kwamba litapambana vilivyo na mashinikizo yote ya kiuchumi, kibiashara na kielimu hadi litakajikomboa kikamilifu kwa miongozo ya busara ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kwa taufiki na uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

No comments:
Post a Comment