Vikosi vya jeshi la Iraq vikishirikiana na vikosi vya kujitolea
vya wananchi vinasonga mbele kuelekea mji wa Al Ramadi, wiki moja baada
ya mji huo kushikiliwa na wanamgambo wa kundi la kigaidi na kitakfiri la
Daesh. Afisa mmoja wa Polisi na mpiganaji wa makabila ya Kisuni
wamesema, kwa msaada wa wanamgambo wa Kishia, vikosi vyao vimeukomboa
mji wa Husaiba al-Sharqiya ulioko umbali wa kilomita 10 mashariki mwa Al
Ramadi kutoka mikononi mwa magadi wa Daesh. Amir al-Fahdawi, kamanda wa
vikosi vya makabila ya Iraq amesema, leo wameukomboa mji wa Husaiba
al-Sharqiya, huku wakiandaa mikakati ya kuwarejesha nyuma zaidi
wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh. Kwa mujibu wa kamanda huyo,
ndege za kivita za jeshi la Iraq zinaendelea kuzishambulia kwa makombora
ngome za kundi la kigaidi la Daesh zilizoko kwenye ufukwe wa Mto
Euphrates. Kushikiliwa mji wa Al Ramadi na kundi la kigaidi la Daesh
kumetilia shaka athari za mashambulio ya anga dhidi ya ngome za kundi
hilo yanayofanywa na muungano wa madola ya kigeni yanayoongozwa na
Marekani. Wakati huo huo Muwaffaq al Rabei, mjumbe wa Kamisheni ya
Usalama na Ulinzi katika bunge la Iraq amesisitiza kuwa mapambano dhidi
ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh yataendelea. Al Rabei amesema
mji mkuu wa Iraq, Baghdad uko salama na kwamba kundi la kigaidi la Daesh
halina uwezo wa kutia mguu katika mji huo
No comments:
Post a Comment