Monday, 11 May 2015
UNICEF: Hali ya kibinadamu Yemen ni mbaya
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetahadharisha
kuhusiana na hali mbaya ya kibinadamu inayoikabili Yemen kutokana na
uvamizi na mashambulio ya kijeshi ya Saudi Arabia katika nchi hiyo na
kusisitiza kwamba, hali ya kibianadamu nchini humo ni mbaya mno. Mohamed
al-Asadi, msemaji wa Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF)
nchini Yemen amesema kuwa, hali ya kibinadamu nchini Yemen inazidi kuwa
mbaya siku baada ya siku. Amesema, kutokana na mashambulio ya Saudia
kusababisha hasara kubwa, hali ya kibinadamu ni mbaya na kwamba,
wananchi wa nchi hiyo wanahitajia misaada zaidi. Tume ya kuchunguza
hasara zitokanazo na mashambulizi hayo, imetangaza kuwa zaidi ya watu
2,000 wamekwishauawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa. Hayo yanajiri
katika hali ambayo, wanajeshi wa Yemen pamoja na wapiganaji wa harakati
ya wananchi ya Ansarullah wamekaribisha kwa mikono miwili pendekezo la
usitishwaji mapigano kwa muda ili kuruhusu misaada ya kibinadamu
kuwafikia raia wa kawaida wanaokabiliwa na matatizo. Usitishaji vita huo
wa siku tano utaanza kutekelezwa kesho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment