Monday, 11 May 2015
Zarif: Iran kupanua ushirikiano wake na Afrika Kusini
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa, Jamhuri ya
Kiislamu iko tayari kustawisha zaidi ushirikiano wake na Afrika Kusini
katika nyanja zote hususan uga wa kiuchumi. Dakta Muhammad Javad Zarif
amesema hayo katika mazungumzo yake na Bi Maite Nkoana-Mashabane, Waziri
wa Mashauri ya Kigeni wa Afrika Kusini ambaye yuko safarini hapa nchini
na kuongeza kuwa, licha ya kuweko vikwazo, lakini Iran na Afrika Kusini
zinaweza kuwa na ushirikiano katika masuala ya mafuta na kadhalika. Kwa
upande wake Bi Maite Nkoana-Mashabane, amesema kuimarishwa ushirikiano
wa Tehran na Pretoria ni jambo muhimu na kwamba, lengo la safari yake
hapa nchini ni katika kuimarisha uhusiano huo. Aidha akizungumza kwenye
kikao cha kamisheni ya pamoja ya uchumi ya Iran na Afrika Kusini Bi
Nkoana-Mashabane alisema vikwazo ilivyowekewa Iran si vya kimantiki, vya
upande mmoja na havina uhalali wa kisheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment