Friday, 8 May 2015
Magaidi Syria waungana kupambana na kundi la Daesh
Makundi ya kigaidi kusini mwa Syria
yameungana na kutekeleza mashambulizi makali dhidi ya wanachama wa kundi
la kigaidi na kitakfiri la Daesh nchini humo. Habari kutoka kwa magaidi
hayo, zimeeleza kuwa, kundi la kitakfiri la Jab’hatu Nusra na makundi
mengine yanayopigana dhidi ya serikali halali ya Syria, yaliungana siku
chache zilizopita na kutekeleza operesheni kali dhidi ya wanachama wa
kundi la Daesh katika eneo la al-Qahtwaniyyah, katika viunga vya mji wa
al-Qunaitra, kusini mwa Syria na kufanikiwa kudhibiti ngome muhimu ya
wanachama wa kundi hilo. Katika mapigano hayo makali, makumi ya
matakfiri wa kundi la Jab’hatu Nusra na Daesh, wameangamizwa huku
wengine wengi wakijeruhiwa vibaya. Makundi hayo ya kitakfiri
yaliyoungana katika operesheni za kuitwaa ngome hiyo muhimu ya kundi la
kigaidi la Daesh, ni pamoja na makundi ya kigaidi ya Jayshul-Islami,
Jayshul-Yarmuuk, Jayshul-Awwal na Ahrarush-Sham, yote ya Masalafi wa
Kiwahabi ambayo yanapambana dhidi ya serikali ya nchi hiyo. Kwengineko
jeshi la Syria kwa kushirikiana na wanamapambano wa Harakati ya Kiislamu
ya Hizbullah, limefanikiwa kudhibiti kikamilifu maeneo ya Isal al-Ward
lenye upana wa kilometa mraba 45 katika mipaka ya pamoja kati ya Syria
na Lebanon, al-Qaranah, Wadi al-Dar na Wadi al-Sahrij, yaliyoko katika
miinuko ya al-Qalamun nchini Syria. Katika operesheni za kudhibiti
maeneo hayo, makundi ya magaidi wa kundi la Jab’hatu Nusra, wakiwamo Abu
Mujahid na al-Aswad, makamanda wa ngazi za juu wa kundi hilo,
wameangamizwa na jeshi la nchi hiyo na wanamapambano wa Hizbullah ya
Lebanon
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment