Mkuu wa kundi linalojiita "Muungano wa Kitaifa wa Wapinzani wa
Nje ya Syria" ameishukuru Marekani kwa kuyasaidia kifedha makundi ya
waasi wa nchi hiyo na kuiomba iendelee kuwa pamoja na waasi hao kwa hali
na mali.
Shirika la habari la Ufaransa limemnukuu Khaled Khoja
akisema hayo jana wakati alipoona na John Kerry, Waziri wa Mambo ya Nje
wa Marekani na kuongeza kuwa, anaishukuru mno Marekani kwa kutoa msaada
wa dola bilioni 3 kwa waasi wa Syria ambao uliwezesha kuanzishwa vita
dhidi ya serikali ya Damascus.
Khaled Khoja ameongeza kuwa, waasi wa
Syria wanaiomba Marekani iwasaidie kuzuia mashambulizi ya serikali ya
Damascus ya kukomboa maeneo yanayodhibitiwa na waasi.
Mkuu huyo wa
wapinzani wa Syria walioko nje ya nchi hiyo aidha amefumbia macho jinai
zinazoendelea kufanywa na makundi ya kigaidi na uungaji mkono wa kila
hali wa Marekani kwa makundi hayo ya kigaidi na kudai kuwa Rais Bashar
al Assad hana uhalali wa kuwa Rais wa nchi hiyo licha ya wananchi wa
Syria kumchagua kwa kura nyingi
No comments:
Post a Comment