Mwanachama wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi na
kitakfiri la Daesh ametiwa mbaroni nchini Lebanon huku akiwa na pasi
bandia ya kusafiria. Ibrahim al Barakat alitiwa mbaroni mapema jana na
anatuhumiwa kwa kuwa wakala wa kundi la kigaidi la Daesh. Hayo
yameelezwa na afisa usalama wa Lebanon. Barakat alitiwa mbaroni wakati
alipokuwa akijaribu kuelekea Uturuki kupitia kaskazini mwa Lebanon huku
akitumia pasipoti bandia.
Mbali na kuvishambulia vikosi vya Lebanon mwaka jana,
Ibrahim al Barakat aliye na umri wa miaka 40 anakabiliwa na tuhuma za
kuwasajili vijana kutoka Tripoli, mji mkubwa zaidi huko kaskazini mwa
Lebanon, kwa ajili ya kupigana na wanamgambo huko Syria na Iraq. Tarehe
11 mwezi Oktoba mwaka jana, wanajeshi 11 wa Lebanon waliuliwa baada ya
mapigano kuzuka kufuatia kutiwa mbaroni raia mmoja wa Lebanon aliyekuwa
akituhumiwa kuwasajili vijana kujiunga na makundi ya kigaidi huko Syria.
No comments:
Post a Comment