Mjumbe wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa umoja huo umeshindwa
kuyashawishi makundi hasimu nchini Libya kufanya mazungumzo baina yao.
Mjumbe huo wa Umoja wa Mataifa nchini Libya ameyapa makundi ya Libya
muda wa wiki moja yahakikishe kuwa yametangaza misimamo yao kuhusiana na
muswada wa makubaliano ya amani yaliyopendekezwa na Umoja wa Mataifa.
Bernardino Leon amesema kuwa, ana matumaini makubaliano hayo yataandaa
mazingira mazuri ya kupatikana amani ya kudumu nchini Libya. Hata hivyo
wanamgambo wa Fajr ambao wanaudhibiti mji mkuu Tripoli jana waliutaka
Umoja wa Mataifa umuondoe mjumbe wake huyo nchini Libya. Aidha
wanamgambo hao wamewataka wakazi wa Tripoli wajitokeze kwa wingi leo
Ijumaa katika maandamano ya kupinga hatua ya Umoja wa Mataifa ya
kuingilia mgogoro wa Libya. Kundi hilo pia limepinga waziwazi mwito wa
Bernadino Leon, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Libya wa kuyataka
makundi hasimu yarejee kwenye meza ya mazungumzo ya amani. Mwezi
Septemba mwaka 2014 Umoja wa Mataifa ulianza rasmi kupatanisha mgogoro
wa Libya baina ya jeshi na wanamgambo wa nchi hiyo hata hivyo mapigano
ya mara kwa mara yamekuwa yakikwamisha juhudi hizo za Umoja wa Mataifa.
No comments:
Post a Comment