Friday, 8 May 2015
Daesh wagawa madawa ya kulevya kwa vijana wa Iraq
Duru za habari kutoka Iraq,
zimeripoti kuwa, kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh limekuwa
likigawa madawa ya kulevya kwa vijana wa nchi hiyo ili kuwafanya waweze
kujiunga na kundi hilo katika kutekeleza jinai za kigaidi. Hayo
yamethibitishwa na Farhan Muhammad, kiongozi mwandamizi wa Baraza la
Mkoa wa al-Anbar na kuongeza kuwa, baada ya kundi hilo la kigaidi
linalotenda jinai kwa jina la Uislamu, kuingiza idadi kubwa ya madawa ya
kulevya ya aina mbalimbali vikiwemo vidonge kupitia mipaka ya Syria
kuelekea al-Anbar, wanachama wa Daesh, wamekuwa wakigawa madawa hayo ya
kulevya kwa vijana wa mkoa huo kitendo kinachotajwa kuwa ni njia
mojawapo ya kuweza kuwafanya vijana wengi wajiunge nalo. Kwa mujibu wa
afisa huyo wa serikali, kundi la Daesh, linatekeleza mpango wa kuwatia
kasumba vijana, sanjari na kuwatumia katika kutekeleza jinai zake hapo
baadaye. Amewataka viongozi wa kundi hilo linalojinadi kuwa na
mafungamano na Uislamu kutekeleza jukumu lao la kidini, badala ya kwenda
kinyume na misingi ya dini hiyo tukufu inayopiga marufuku vitendo vya
aina hiyo. Hayo yanajiri katika hali ambayo, hivi karibuni kulienea
habari kwamba, wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh
wamekuwa wakitumia vidonge vya kulevya ili kuwafanya wasipitiwe na
usingizi vitani. Mbali na hapo hivi karibuni pia kundi hilo liliifanyia
matengenezo hoteli ya kimataifa ya Nainawa iliyopo katika mji wa Mosul
nchini Iraq ambayo itatumiwa na makamanda wake katika starehe na anasa.
Mambo hayo pamoja na mengineyo, ndiyo yaliyowafanya weledi wa mambo
waamini kuwa, kundi hilo kinyume na madai yake, linakwenda kinyume na
misingi ya Kiislamu na linatekeleza njama za Wamagharibi dhidi ya dini
hiyo tukufu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment