Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema magaidi hawatafanikiwa
katika njama zao za kuvuruga azma ya Wasyria katika mapambano yao dhdi
ya ugaidi.
Assad ameyasema hayo Jumatano mjini Damascus katika mkutano na
Alaeddin Boroujerdi, Mkuu wa Kamati ya Usalama wa Taifa na Sera za
Kigeni katika Bunge la Iran, Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu.
Katika kikao hicho, Assad na Boroujerdi walijadili na kuashiria
uungaji mkono wanaopata magaidi kutoka baadhi ya nchi za Magharibi na
waitifaki wao katika eneo na kusema magaidi ni vibaraka wa nchi
zinazowaunga mkono. Rais wa Syria amesema magaidi na waungaji mkono wao
wamekuwa wakifanya hadaa na kueneza propaganda ili kufidia kipigo
wanachopata katika medani ya vita. Amesema kwa irada yao imara na msaada
wa nchi rafiki kama Iran, Wasyria wanaangamiza ugaidi na machafuko
katika nchi yao. Kwa upande wake Boroujerdi amewapongeza Wasyria, jeshi
na uongozi wa nchi hiyo kwa kusimama imara na kuongeza kuwa, wakiendelea
hivyo hatimaye watapata ushindi kamili dhidi ya magaidi. Aidha amesema
Iran itaendelea kuiunga mkono Syria hadi pale mgogoro utakapomalizika
nchini humo. Wakati huo huo duru za habari zinasema wapiganaji wa
Harakati ya Hizbullah ya Lebanon wamepata mafanikio makubwa katika
mapamabano na magaidi katika milima ya Qalamoun kaskazini mwa Damascus
No comments:
Post a Comment