Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imetangaza
kuwa ipo tayari kushiriki katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa bunge na
urais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina. Hamas imetoa taarifa na
kutangaza utaarifu wake kwa ajili ya kushiriki katika uchaguzi wa
Palestina na kumtuhumu Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya
Palestina kuwa ndiye anayekwamisha utekelezaji wa mchakato wa kisheria
wa uchaguzi. Taarifa ya Hamas imeongeza kuwa Mahmoud Abbas halipi uzito
wa hali ya juu suala la kufanyika uchaguzi na anakwamisha kuainishwa
tarehe ya kufanyika chaguzi hizo. Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya
Palestina Hamas vile vile imeshutumu matamashi ya Mahmoud Abbas kwamba
upo ulazima kwa Hamas kuwasilisha ombi la kimaandishi kwa ajili ya
kufanyika uchaguzi huo na kuongeza kuwa matamshi hayo ni wazi
yatazidisha mgawanyiko kati ya Wapalestina na kukwamisha kufikiwa
makubaliano na mapatano ya kitaifa.
No comments:
Post a Comment