Rais Milos Zeman wa Czech amesema kuwa vikwazo vilivyowekwa kwa
Russia kutokana na mgogoro wa Ukraine havina athari bali vinachochea
hali ya mivutano. Rais wa Czech amesema kuwa vikwazo vya Magharibi dhidi
ya Russia havina athari, bali vimekuwa tu vikizidisha hali ya mivutano
na ametaka kuondolewa vikwazo hivyo haraka iwezekanavyo.
Madola ya Magharibi yameiwekea Russia vikwazo ka kuituhumu nchi hiyo
kwamba inahusika katika mgogoro mkubwa wa hivi sasa katika nchi jirani
ya Ukraine; mgogoro ulioibuka baada ya Kiev kuanzisha oparesheni za
kijeshi dhidi ya vikosi waitaki wa Russia mashariki mwa Ukraine mwaka
uliopita. Russia imekanusha tuhuma hizo za Magharibi dhidi yake
No comments:
Post a Comment