Watu wasiopungua tisa wameuawa na wengine wengi
kujeruhiwa baada ya ndege za kivita za Saudia kudondosha mabomu licha ya
utawala huo wa Riyadh kutangaza usitishaji wa hujuma yake ya kijeshi ya
wiki saba dhidi ya nchi hiyo masikini.
Duru zinaarifu kuwa Wayemen kadhaa wameuawa leo baada ya
ndege ya helikopta aina ya Apache kushambulia eneo la al-Safiya katika
mkoa wa Sa'ada kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Hali kadhalika mapema
leo ndege za kivita za Saudia zimedondosha mabomu katika bandari ya Aden
na mikoa ya Hajjah na Abyan. Saudia imekiuka tangazo lake la usitishaji
vita kwa muda wa siku tano kuanzia Jumanne. Wakati huo huo Iran imesema
meli yake inayopelekea misaada ya kibinadamu Yemen imefanya hivyo kwa
ushirikiano na Umoja wa Mataifa. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran
anayeshughulikia masuala ya Kiafrika na Kiarabu Hossein Amir-Abdollahian
amesisitiza kuwa meli hiyo ya misaada ya Iran itafika Yemen kama
ilivyopangwa. Hivi karibuni Kamanda mwandamizi wa jeshi la Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran alitahadharisha kuwa, shambulizi lolote dhidi ya meli
ya misaada ya kibinadamu ya Iran inayoelekea Yemen litawasha moto wa
vita katika eneo zima la Mashariki ya Kati. Jenerali Masoud Jazayeri,
amesema meli hiyo iliyopewa jina la 'Nejat' yaani 'uokovu' imebeba
misaada ya kibinadamu kama vile chakula na dawa na wala haipaswi kuzuiwa
au kushambuliwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa
No comments:
Post a Comment