Meli ya misaada ya kibinadamu ya Iran kwa ajili ya wananchi
wanaondelea kushambuliwa kinyama na Saudi Arabia huko Yemen inaendelea
na safari yake baada ya kuondoka katika bandari ya Bandar Abbas, kusini
mwa Iran.
Meli hiyo ya mizigo iliyopewa jina la Nejat yaani "wokovu"
ina tani 2,500 za mahitaji ya lazima zaidi kikiwemo chakula, madawa na
mahema.
Mbali na maafisa wa Hilal Nyekundu ya Iran, wanaharakati
kadhaa wa kimataifa wamo ndani ya meli hiyo. Kati ya wanaharakati hao
wako wafanyakazi wa kutoa misaada ya kibinaadamu, hudumza za afya na
wanaharakati wa kutetea amani kutoka Marekani, Ufaransa na Ujerumani.
Waandishi wa habari na timu ya madaktari kutoka Iran ni miongoni mwa watu waliomo kwenye meli hiyo.
Meli
hiyo itapitia Lango Bahari la Hormuz, Ghuba ya Oman, Bahari Arabu na
yamkini ikatia nanga katika Ghuba ya Aden au kuelekea Bandari ya
Hudaydah. Wakati huo huo Sayyid Amir Mohsen Zeyai, mkuu wa shirika la
Hilal Nyekundu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelilaumu vikali shirika
la kimataifa la Msalaba Mwekundu kwa kudharau masaibu yanayoendelea
kuwatesa wananchi wasio na hatia wa Yemen
No comments:
Post a Comment