Ban Ki moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa
anasikitishwa na hatua ya Saudi Arabia ya kuendeleza mashambulizi nchini
Yemen.
Ban alisema hayo jana na kuongeza kuwa, mashambulizi dhidi ya
raia na miundombinu isiyo ya kijeshi zikiwemo hospitali na maeneo ya
Umoja wa Mataifa nchini Yemen hayakubaliki kabisa na ni uvunjaji wa wazi
wa haki za binadamu.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametosheka tu
na kusema anasikitishwa na jinai hizo za Saudi Arabia nchini Yemen
katika hali ambayo mashambulizi dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu
yameendelea kusababisha maafa kwa watu wasio na hatia.
Karibu watu 1,000 wameshauwa katika mashambulizi ya Saudia nchini Yemen wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wadogo.
Jana
pia ndege za Saudi Arabia zilishambulia ofisi za televisheni ya al
Masirah ambayo inahesabiwa kuwa marejeo makubwa ya habari zinazohusiana
na mashambulizi ya Saudia nchini Yemen
No comments:
Post a Comment