Uongozi wa operesheni za kijeshi za Dijla nchini Iraq umetangaza
kuwa, vikosi vya nchi hiyo vimefanikiwa kukomboa kikamilifu kisima cha
mafuta cha Ajil, mashariki mwa mji wa Tikrit baada ya kupambana vikali
na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh na kuua wanamgambo 73.
Vyombo
vya habari vya Iraq vimemnukuu Luteni Jenerali Abdul Amir al Zaydi
akisema kuwa, mapigano makali yalizuka baina ya vikosi vya Iraq na
wanamgambo wa Daesh na kupelekea wanamgambo 73 kuuawa wakiwemo wenye
uraia wa kigeni.
Luteni Jenerali al Zaydi ameongeza kuwa, askari
watatu wa vikosi vya ulinzi vya Iraq wameuawa na wengine 13 kujeruhiwa
katika mapambano hayo.
Vikosi vya ulinzi vya Iraq vimefanikiwa pia kuangamiza magari 37 ya kivita ya kundi la kigaidi la Daesh.
Ameongeza
kuwa, kisima hicho cha mafuta kilichovamiwa na wanamgambo wa Daesh
kinadhibitiwa kikamilifu na vikosi vya ulinzi vya Iraq hivi sasa
No comments:
Post a Comment