Tuesday, 12 May 2015
Televisheni ya al Masirah yaonesha ndege ya Morocco
Televisheni ya al Masirah ya nchini Yemen imerusha hewani mkanda
wa video unaoonesha ndege yenye bendera ya Morocco iliyoangushwa na
wanamapambano wa kikabila wa Yemen kaskazini mwa nchi hiyo. Katika
mkanda huo wa video, anaonekana mwandishi wa televisheni hiyo akionesha
baadhi ya mabaki ya ndege hivyo ambapo katika sehemu moja ya mabaki hayo
ya ndege kunaonekana pia bawa la ndege lenye bendera ya Morocco.
Wapiganaji wa kikabila wanaonekana wakishingiria na kukusanya mabaki ya
ndege hiyo ya kijeshi ya Morocco aina ya F16 iliyokuwa inafanya
mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen. Huku hayo yakiripotiwa, Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya Afrika na
Kiarabu, Hussein Amir Abdollahiyan amesema kuwa kinachotarajiwa kutoka
kwa Umoja wa Mataifa ni kuchukua hatua za maana za kukomesha uadui wa
Saudi Arabia dhidi ya wananchi wa Yemen. Bw. Abdollahiyan alisisitiza
hayo katika mazungumzo ya simu baina yake na mjumbe mpya wa Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa katika kadhia ya Yemen, Bw. Ismail Ould Cheikh
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment