Friday, 15 May 2015
Rwasa: Burundi inakaribia tena vita vya ndani
Kiongozi wa chama cha upinzani cha FNL nchini Burundi amesema
nchi hiyo ya Afrika Mashariki inakaribia kutumbukia tena kwenye vita vya
ndani na ameitaka jamii ya kimataifa kuingilia kati ili suala hilo
lisitokee. Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na idhaa hii mapema leo,
Agathon Rwasa amesema jeshi la Burundi linaonekana kugawanyika baada ya
tangazo lililotolewa hapo jana na Jenerali Godefroid Niyombare, kwamba
ameipindua serikali ya Rais Pierre Nkurunziza. Bw. Rwasa amesema iwapo
mapinduzi ya kijeshi yanayoendelea yatakosa kufanikiwa na Rais
Nkurunziza akarudi madarakani na kudhibiti hali ya mambo, kiongozi huyo
atahitajika kutumia fursa hiyo kufungua milango ya mazungumzo badala ya
kutumia mkono wa chuma dhidi ya mahasimu wake. Kiongozi wa chama cha FNL
pia amesema iwapo mapinduzi yatafanikiwa, wafanyamapinduzi watapaswa
kujumuisha Warundi wote katika mchakato wa kurudisha utawala wa sheria
haraka iwezekanavyo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment