Tuesday, 12 May 2015
Pakistan yatuma askari usalama nchini Bahrain
Viongozi wa Pakistan wametangaza kuwa wametuma askari maalumu wa
masuala ya kiusalama nchini Bahrain baada ya kuombwa na viongozi wa ukoo
wa kifalme wa Aal Khalifa ili kupambana na wimbi la mapinduzi la
wananchi wa nchi hiyo. Shirika la habari la Reuters limezinukuu duru za
Pakistan zikifichua jana kuwa, askari maalumu wa masuala ya kiusalama wa
Pakistan wametumwa nchini Bahrain ili kushirikiana na mamluki kutoka
nchi nyinginezo kwa ajili ya kuzima harakati za kimapinduzi za wananchi
wa nchi hiyo. Hayo yameripotiwa katika hali ambayo wachambuzi wa masuala
ya kisiasa wanaamini kuwa, si jambo rahisi kuweza kuzimwa harakati hizo
za wananchi wa Bahrain hasa kutokana na kuwa, Saudia ambayo imetuma
wanajeshi wake kukandamiza wananchi wa Bahrain, hivi sasa inafanya jinai
pia katika nchi nyingine ya Kiarabu na Kiislamu ya Yemen. Vile vile
utawala wa kifalme wa Bahrain unaendelea kumshikilia Sheikh Ali Salman,
Katibu Mkuu wa chama cha Kiislamu cha al Wifaq cha nchi hiyo pamoja na
Nabil Rajab, mwanaharati wa haki za binadamu wa Bahrain. Utawala wa ukoo
wa Aal Khalifa huko Bahrain umeomba msaada kutoka kwa Marekani, Saudi
Arabia na baadhi ya nchi kama vile Pakistan ili kuzima harakati za
wananchi wa nchi hiyo wanaopigania haki zao na kuupinga utawala huo wa
kiimla
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment