Friday, 1 May 2015
Kiongozi wa waasi wa ADF atiwa mbaroni nchini TZ
Habari kutoka nchini Tanzania zinasema kuwa, kiongozi wa kundi la
waasi wa ADF wa nchini Uganda ametiwa mbaroni nchini Tanzania. Vyombo
vya habari yakiwemo magazeti ya nchini Uganda yamethibitisha kutiwa
mbaroni mtu anayeaminiwa kuwa ni Jamil Mukulu, mkuu wa kundi la waasi wa
ADF ambao wanatuhumiwa kufanya mauaji ya watu 300 tangu mwezi Oktoba
hadi hivi sasa katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Habari zinasema kuwa Mukulu ametiwa mbaroni kwa ushirikiano wa polisi wa
Tanzania na wenzao wa Uganda. Hata hivyo jeshi la Uganda limesema kuwa
haliwezi kuthibitisha kuwa mtu aliyetiwa mbaroni ni Jamil Mukulu hadi
atakapochukuliwa vipimo vya vinasaba, DNA. Kwa muda mrefu polisi ya
Uganda ilikuwa imetoa amri ya kutiwa mbaroni kiongozi huyo wa waasi wa
ADF mwenye umri wa miaka 51 kwa tuhuma za kufanya mauaji ya kigaidi na
kuiomba Interpol iisaidie kutiwa mbaroni kiongozi huyo wa waasi. Kundi
la ADF lilianzishwa mwaka 1995 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo ili kupambana na siasa za Rais Yoweri Museveni wa Uganda
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment