Jeshi la Nigeria limetangaza amri ya kutotoka nje (curfew) katika
mji wa Maiduguri kaskazini mashariki mwa nchi hiyo siku moja baada ya
wapiganaji wa Boko Haram kuvamia mji huo. Msemaji wa jeshi la Nigeria,
Kanali Tanko Gusau, amesema hatua hiyo imechukuliwa ili kuwalinda raia
na mali zao. Wakaazi wa Maiduguri watatakiwa kubakia majumbani mwao
kuanzia saa 12 jioni hadi 12 asubuhi kila siku hadi hali itakapoimarika.
Hapo jana Jumatano, wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram walivamia mji wa Maiduguri lakini jaribio lao la kuteka kambi ya kijeshi katika mji huo lilifeli baada ya kuzidiwa nguvu na wanajeshi wa serikali. Habari zinasema wanajeshi 3 waliuawa kwenye mapigano ya hapo jana huku Boko Haram likipoteza makumi ya wapiganaji wake. Pia vijana 6 wa kujitolea wanaolinda mji wa Maiduguri maarufu kama sungusungu wamepoteza maisha kwenye patashika hiyo

No comments:
Post a Comment