Saudi Arabia leo imelazimika kutangaza hali ya hatari katika
ukanda wa mpaka wake wa kusini na Yemen baada ya kuongezeka mashambulizi
ya makombora ya wanamapambano wa Yemen dhidi ya Saudia.
Televisheni
ya al Masirah imetangaza kuwa, jeshi la Yemen na wapiganaji wa kamati za
wananchi wa nchi hiyo wameendelea kushambulia maeneo ya Saudia
yanayopakana na mkoa wa Saada, kama ambavyo wameshambulia kwa makombora
pia jengo la walinzi wa mpakani wa Saudia katika eneo la at Twiwaal huko
Jizan.
Wakati huo huo wakazi wa mkoa wa al Jawf wa kaskazini mwa
Yemen wameandamana kulalamikia uongo unaoenezwa na televisheni za al
Jazeera na al Arabiya. Televisheni ya al Masirah imeripoti kuwa,
wananchi wa Yemen leo wameandamana katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa
mpakani wa al Jawf kaskazini mwa Yemen wakikanusha na kulalamikia uongo
unaonezwa na televisheni hizo za Qatar na Saudia kwamba eti wakazi wa
mkoa huo wako tayari kupambana na Ansarullah. Waandamanaji wamesema
kuwa, uongo kama huo hautatia doa mshikamano wa wananchi wote wa Yemen
katika kukabiliana na jinai wanazofanyiwa na Saudia na waitifaki wake
No comments:
Post a Comment