Duru za kuaminika zimefichua kuwa, Saudi Arabia na utawala wa
Kizayuni wa Israel zimetiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kijasusi
katika suala la Yemen pamoja na kutumiwa ndege zisizo na rubani za
Kizayuni katika anga ya Yemen. Mwandishi wa Radio Tehran amezinukuu duru
za kuaminika zikifichua kuwa, Khalid bin Ali bin Abdullah al Hamidan,
mkuu wa shirika la kijasusi la Saudi Arabia hivi karibuni alielekea
katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na kutia
saini mkataba wa ushirikiano wa kijasusi kati ya Saudia na utawala wa
Kizayuni wa Israel. Kabla ya hapo baadhi ya vyombo vya habari kama vile
televisheni ya al Alam na gazeti la Kizayuni la Yediot Ahronot
vilitangaza habari ya kutua ndege ya Saudi Arabia katika uwanja wa ndege
wa Ben-Gurion huko Tel Aviv. Mashirika ya habari yalisema kuwa ndege
hiyo ilikuwa ya mwana mmoja wa ukoo wa kifalme wa Aal Saud ingawa Saudia
ilidai kuwa ndege hiyo ilikuwa na shirika la ndege la Ureno. Hii si
mara ya kwanza kuripotiwa habari za ushirikiano baina ya utawala wa
Kizayuni wa Israel na ukoo wa Aal Saud na habari za kuweko ushirikiano
mpya baina ya pande hizo mbili dhidi ya wananchi wa Yemen zinatilia
nguvu ushirikiano wa muda mrefu baina ya Saudia na utawala wa Kizayuni
wa Israel.
No comments:
Post a Comment