Monday, 11 May 2015
Kikwete aitisha mkutano wa EAC kuijadili Burundi
Rais Jakaya Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameitisha
mkutano wa wakuu wa nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ili
kujadili mgogoro unaoikabili Burundi. Rais Kikwete ameitisha mkutano huo
wakati Burundi ikiripotiwa kuwa katika vurugu zinazotishia hali ya
usalama, hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi ujao.
Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Kiduru wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) amesema kuwa, kuna haja ya kufanyika mkutano huo kwa
ajili ya kujadili mgogoro wa kisiasa unaoikabili Burundi. Rais Kikwete
amesema kama ninavyomnukuu: “Tumekubaliana kuwa sisi ndani ya EAC yaani
Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi yenyewe tukutane Dar es
Salaam, Jumatano ya keshokutwa, ili tujadiliane jinsi gani ya kuwasaidia
ndugu zetu wa Burundi kuandaa uchaguzi wao kwa mafanikio, wakihakikisha
kuwa nchi yao inabakia na umoja, utulivu, usalama na amani bila
misukosuko isiyokuwa na sababu. Wakati huo huo, wimbi la wakimbizi wa
Burundi wanaoingia Tanzania linazidi kuongezeka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment