Mamia ya Wamarekani wenye hasira wamemiminika tena kwenye mitaa
ya miji mbalimbali ya nchi hiyo kulalamikia mauaji ya Mmarekani mwenye
asili ya Afrika, Freddie Gray aliyekufa kutokana na majeraha akiwa
mikononi mwa polisi.
Mamia ya Wamarekani jana waliendelea kuandamana katika miji ya Baltimore, Maryland, Philadelphia, Pennsylvania pamoja na Cincinnati na Ohio.
Freddie Gray (25) alikufa tarehe 19 mwezi uliopita wa Aprili kutokana na majeraha makubwa, ikiwa ni wiki moja tu tangu alipotiwa mbaroni na polisi wa mji wa Baltimore. Maafisa sita wa polisi walioshiriki kumtia mbaroni Gray wamesimamishwa kazi.
Waandamanaji walibeba mabango yaliyoandikwa: "Komesha Ugaidi wa Polisi," "Sisi na watoto wetu si wahuni" n.k.
Miji mingi ya Marekani imeshuhudia maandamano katika kipindi cha wiki moja iliyopita na watu wengi wametiwa mbaroni na polisi kwa kushiriki kwenye maandamano hayo. Polisi wamewatia mbaroni zaidi ya watu 120 katika mji wa New York pekee.

No comments:
Post a Comment