Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Friday, 12 December 2014

Wanajeshi 6 wa Afghanistan wauawa kwenye mlipuko

Basi lililokuwa limewabeba wanajeshi wa Afghanistan limeshambuliwa na mlipuaji wa kujitolea kufa viungani mwa mji mkuu, Kabul, ambapo wanajeshi 6 wameuawa na wengine 11 kujeruhiwa. Dawlat Waziri, afisa mwandamizi katika Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan amesema mlipuaji huyo wa kujitolea kufa alikuwa akitembea kwa miguu wakati alipojilipua karibu na basi hilo leo mchana. Kundi la kigaidi la Taliban limedai kuhusika na shambulizi hilo na limesema wanajeshi waliouawa ni 12 na kwamba wengine 13 wamejeruhiwa. Kundi la Taliban pia limedai kuhusika na shambulizi jingine la leo asubuhi dhidi ya soko la umma katika mkoa wa Herat ulioko magharibi mwa Afghanisan. Serikali haijataja idadi ya waliouawa katika shambulizi hilo.
Katika wiki za hivi karibuni kundi la Taliban limeshadidisha mashambulizi dhidi ya majengo ya serikali, hoteli zinazotumiwa na raia wa kigeni pamoja na vituo vya polisi na jeshi ndani na nje ya mji wa Kabul.

No comments:

Post a Comment