Kesi inayomkabili Simone Gbagbo mke wa rais wa zamani wa Ivory
Coast anayetuhumiwa kuvuruga usalama nchini humo, ilianza jana Jumanne
katika mji mkuu wa kiuchumi wa nchi hiyo, Abidjan. Wakili wa Simone
Gbagbo amesema ana matumaini kesi hiyo itafanyika kwa uadilifu.
Inasemekana kuwa, mke huyo wa raia wa zamani wa Ivory Coast amehamishwa
kutoka kaskazini hadi kusini mwa mji huo kwa ajili ya kesi hiyo. Bi.
Simone Gbagbo anatuhumiwa pia na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC)
kutenda jinai dhidi ya binadamu, na mahakama hiyo imetaka ikabidhiwe
mtuhumiwa huyo. Hata hivyo serikali ya Ivory Coast sambamba na
kusisitiza kuwa mahakama za nchi hiyo zina uwezo wa kuhukumu kiadilifu,
imejiepusha kumkabidhi mwanamama huyo.
Wapinzani wa serikali ya Ivory Coast wanasisitiza kuwa Laurent Gbagbo hana hatia na wanataka arejeshwe nchini humo. Tangu Novemba 31 mwaka 2011 kiongozi huyo wa zamani anashikiliwa na mahakama ya The Hague kwa tuhuma za kutenda jinai dhidi ya binadamu. Inaonekana kuwa, viongozi wa Ivory Coast wanalipa kipaumbele suala la kuimarisha amani na utulivu nchini na wanafanya jitihada za kuwavutia wapinzani hasa katika kipindi hiki cha kukaribia uchaguzi uliopangwa kufanyika mwakani.
Weledi wa mambo wanaamini kuwa, kutokana na hali tata ya sasa, itakuwa vigumu kwa rais wa sasa wa nchi hiyo Alassane Ouattara kushinda katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015. Nchi ya Ivory Coast imekuwa ikisumbuliwa na mapigano ya hapa na pale ya kikabili baada ya Ouattara kuchukua hatamu za uongozi. Wachambuzi wa masuala wa kisiasa wanasema kuwa, mwenendo huo unaweza kuitumbukiza tena Ivory Coast katika machafuko ya ndani.
Kwa upande mwingine kushtadi malalamiko ya jumuiya za wafanyakazi ya kupinga umasikini katika jamii, ni kadhia nyingine iliyopunguza umaarufu wa Alassane Ouattara. Inasemekena kuwa, kukithiri umasikini kumeathiri nyanja zote za kimaisha ikiwemo sekta ya afya, lishe, elimu na makazi ya wananchi wa Ivory Coast.
Tatizo jingine linalozididisha hali ya ukosefu wa usalama nchini humo ni kuwepo idadi kubwa ya silaha mikononi mwa raia. Tangu wakati wa uasi wa mwaka 2002 na vita vya ndani vya mwaka 2010 hadi 2011, takriban silaha nyepesi laki moja zimebakia mikononi mwa raia. Baadhi wanasema kuwa, silaha hizo ndizo zinazosababisha machafuko na mauaji nchini Ivory Coast. Hivi karibuni taasisi moja ya Afrika iliitaka serikali ya Abidjan ifanye jitihada zaidi kwa ajili ya kuharakisha mwenendo wa kukusanya silaha nyepesi miongoni mwa raia.
Weledi wa mambo wanasema kwamba, viongozi wa nchi hiyo, wanajitahidi kulegeza misimamo na kutochukua hatua kali dhidi yawapinzani kwa kuzingatia hali ya mambo inayotawala nchini humo. Hasa kwa kuwa, chama cha upinzani cha Ivorian Popular Front (IPF) ambacho kinaendelea kumuunga mkono Gbagbo huenda kikawa na taathira katika matokeo ya uchaguzi ujao. Kwa kuzingatia hayo yote, baadhi wanaamini kuwa, ni jambo lililo mbali kuwa Simone Gbagbo atapewa adhabu kali kupitia kesi hiyo inayomkabili

No comments:
Post a Comment