Mkuu wa Kitengo cha Intelijinsia nchini Sudan
amesisitiza kuwa vikosi vya usalama vya nchi hiyo vimewekwa tayari kwa
lengo la kukabiliana na vita vya pande zote dhidi ya makundi ya waasi
nchini humo. Muhammad Atta al Mauli amesema kuwa, ulinzi na usalama
unapaswa kuimarishwa zaidi kwa lengo la kukabiliana na makundi ya waasi
yanayoleta chokochoko katika majimbo mbalimbali ya nchi hiyo. Al Mauli
ameongeza kuwa, vikosi vya usalama vimejizatiti katika maeneo ya majimbo
ya Kordofan Kusini na Darfur kwa lengo la kukabiliana na mashambulizi
hayo ya waasi. Amesema kuwa, baadhi ya makundi yanajaribu kuwavunja moyo
wananchi kwa kusambaza fikra na propaganda potovu kwamba jeshi la Sudan
halina uwezo wa kupambana na makundi ya waasi. Inafaa kuashiria hapa
kuwa, majimbo ya Kordofan Kusini na Darfur yanakabiliwa na machafuko kwa
karibu miaka mitatu sasa, tokea Sudan Kusini ilipojitenga na Sudan na
kuwa taifa huru.
No comments:
Post a Comment