MADAI! Huku zikiwa zimepita siku chache tangu igundulike kwamba muigizaji, Aunt Ezekiel kuwa na mimba ambayo inasadikiwa kuwa si ya mume wake (Sunday Demonte), ndugu wa mume huyo wameibuka na kutaka kumfikisha Bakwata (Baraza Kuu la Waislamu Tanzania).
“Ni lazima tulisimamie kidete, haiwezekani mwanamke kaolewa halafu anapata mimba nje ya ndoa, hili suala tutalisimamia na lazima tumfikishe Bakwata,” alisema mmoja wa ndugu.
Alipotafutwa Aunt Ezekiel kulizungumzia hilo, alisema;
“Wanifikishe Bakwata kwa lipi? Kwani nimeolewa na ndugu au Demonte? Hawawezi kunifikisha Bakwata hivyo wasinifuatilie.”
No comments:
Post a Comment