Marekani imeeleza kuwa ilijaribu
kumwokoa raia wake mzaliwa wa Uingereza Luke Somers, anayeshikiliwa
mateka na al-Qaeda nchini Yemen.
Rais Barack Obama aliidhinisha kikosi cha kumwokoa Luke, mwezi uliopita.
“Kwa masikito, Luke hakuwepo, japokuwa mateka kutoka mataifa mengine
walikuwepo na waliokolewa,” Baraza la Usalama la Taifa, limesema.
Mtu anayejitambulisha kama Luke Somers, ambaye alitekwa mwaka 2013,
ameonekana katika video, akisema maisha yake yako hatarini na anaomba
msaada.
Video hiyo pia inamwonyesha mfuasi wa al-Qaeda huko Yemen akitishia
kumuua Bwana Somers hadi madai yao ambayo hayajatajwa, yatakapotimizwa.
Bwana Somers, mwenye umri wa miaka 33, alifanyakazi kama mwandishi wa
habari na mpiga picha wa mashirika ya huko na kazi zake zikaonekana
katika vyombo vya habari vya kimataifa, ukiwemo mtandao wa BBC. Luke Somers raia wa Marekani mwandishi wa habari anayeshikiliwa mateka na al-Qaeda huko Yemen
Familia ya Somers imetoa ombi kwa Al-Qaeeda kuwa na huruma na Somers na kumwachilia.
Mamake Somers alinukuliwa akisema: ” Tafadhali…………tupeni nafasi kumuona Luke kwa mara nyingine.”
Katika kanda iliyowekwa kwenye mtandoa wa You Tube, mamake Somers
pamoja na kakake, wamesema Luke alikuwa tu anajaribu kuwatendea mema
watu wa Yemen. ”
“Luke ni mpiga picha tu na hana hatia ya kufanya chochote kibaya wala
kwa vitendo vinvyofanywa na serikali ya Marekani, ” alisema kakake
Somers.
Mwandishi huyo wa habari alikamatwa mwaka 2013 mwezi Septemba.
Somers, 3mwenye umri wa miaka 33, alifanya kazi kama mpiga picha na
mwandishi na taarifa zake zilitumiwa na mashirika ya kimataifa yua
habari ikiwemo BBC.
No comments:
Post a Comment