Joseph Kapinga
Nilipata wakati mgumu sana mwanangu aliponiuliza
hivi karibuni kuhusu suala la escrow. Aliniuliza: “Mara nyingi nasikia
unazungumza na wenzako ‘eskroo’ ndiyo kitu gani? Hata kwenye televisheni
nasikia sana wanaongelea.”
Kwa utoto wake, sikuwa na jibu lenye maelezo
ambayo yangemfanya kujua kwa undani suala hilo. Tuliachana hapo.
Umaarufu wa sakata la escrow ni mkubwa kuliko maelezo. Hata hivyo,
pamoja na sakata hilo kushika hatamu kila sehemu ya nchi, bado watu wa
mpira tuna mambo yetu ya kuzungumza kila wiki.
Nimesikia eti klabu za Simba na Yanga zinaua vipaji vya wachezaji chipukizi.
Kwa haraka haraka, unaweza kutoa jibu jepesi kwamba ni kweli klabu hizo zinafanya hivyo.
Mimi nisingependa kuwa na jibu jepesi kiasi hicho,
nikiamini kwamba hata wachezaji chipukizi wenyewe wamekuwa sehemu ya
kuua vipaji vyao.
Sababu ni moja tu. Ndoto za chipukizi katika soka
la Bongo ni kucheza Simba au Yanga. Vijana wetu wamejaa utamaduni
unaowafunga kuwa na ndoto za mbali zaidi ya kucheza Simba na Yanga,
ambako wakienda huko huishia kusugua benchi.
Mfano, Nonda Shaban aliichezea Yanga, lakini
dhamira yake haikuwa kubaki Tanzania bali kucheza kwa kiwango cha juu
zaidi. Alifanikiwa.
Mshambuliaji mpya wa Simba, Danny Sserunkuma
nimemsikia akisema kuwa amejiunga na Simba ili kupata fursa ya kutimiza
ndoto yake kucheza soka la kulipwa Ulaya. Tujiulize ni wachezaji
chipukizi wangapi wa Tanzania wenye ndoto za kucheza soka la kimataifa
zaidi ya Simba na Yanga?
Tunaweza kuzilaumu klabu hizi kuwa sehemu ya kuua
vipaji vya vijana wetu, pia tuangalie upande wa pili ambao ni utayari wa
ndoto za chipukizi hao kucheza soka la kimataifa
No comments:
Post a Comment