Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Friday, 12 December 2014

Watu milioni 20 kushiriki Arubaini ya Imam Hussein (as)

Maafisa wa serikali ya Iraq wamesema kuwa inakadiriwa watu milioni 20 watashiriki katika maombolezo ya siku ya Arubaini ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) Imam Hussein (as) katika mji mtakatifu wa Karbala Jumamosi ya kesho.
Waislamu wa madehebu ya Shia kutoka nchi mbalimbali dunia wanaendelea kuwasili katika mji huo mtakatifu kwa njia mbalimbali za usafiri wa anga na nchi kavu kukumbuka siku ya Arubaini na tukio chungu la kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) akigapania dini ya Mwenyezi Mungu na matukufu ya kibinadamu hapo mwaka 61 Hijria. Serikali ya Iraq imetangaza kuwa hadi sasa Waislamu milioni 17 wamewasili mjini karbala na kwamba inatarajiwa kuwa idadi ya watu wanaokwenda kuzuru kaburi la Imam Hussein itafikia milioni 20 hadi Jumamosi ya kesho.
Jeshi la Iraq limeimarisha usalama katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo hususan mjini Karbala kwa kuhofia mashambulizi ya kundi la kigaidi na kiwahabi la Daesh.
Maombolezo ya siku ya Arubaini hufanyika kila mwaka baada ya kupita siku Arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya Imam Hussein AS na masahaba zake 72 ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbala mnamo mwaka 61 Hijria

No comments:

Post a Comment