Duru za habari kutoka Afrika Kusini zimetangaza kufichuliwa
utajiri mkubwa na dafina iliyofichwa wakati wa kipindi cha utawala wa
dikteta Muammar Gaddafi wa Libya nchini humo. Gazeti la Independent
Online la nchini Afrika Kusini limeandika kuwa, zaidi ya dola bilioni
200, mamia ya tani za dhahabu, vipande milioni sita vya almasi na vito
vya thamani vilitoroshwa na utawala wa Gaddafi na kuhamishiwa nchini
Afrika Kusini. Taarifa zinasema kuwa, mali zote zilizotoroshwa na
utawala wa dikteta Gaddafi nchini Afrika Kusini zimehifadhiwa kwenye
maghala saba, na zinafikia zaidi ya dola trilioni mbili. Gazeti hilo
limeandika kuwa, Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na serikali yake
wanakabiliwa na mashinikizo makubwa ya jamii ya kimataifa kuhusiana na
mali na utajiri huo mkubwa wa wananchi wa Libya uliofichwa nchini humo.
Imeelezwa kuwa, hivi sasa dafina hiyo iliyoibiwa kutoka Libya na
kufichwa katika eneo la siri lililoko katika maeneo ya kati ya
Johannesburg na Pretoria ilisafirishwa kwa kutumia zaidi ya shehena 62
za ndege kutoka Libya na kupelekwa Afrika Kusini mwishoni mwa utawala wa
dikteta Gaddafi
No comments:
Post a Comment