Serikali mpya ya Afghanistan imeanza kupata sura baada ya Rais Ashraf Ghani kuwaarifisha mawaziri wanne muhimu.
Rais Ghani leo Ijumaa amewaarifisha Muhammad Mastur (Fedha), Mujghan Mustafawi (Masuala ya Wanawake), Muzamil Shinawari (Biashara) na Atikullah Atif Mal kama Waziri wa Mambo ya Nje. Hatua hiyo ya Rais mpya wa Afghanistan imechukuliwa baada ya kupita zaidi ya mwezi mmoja tangu kiongozi huyo akubali kugawana madaraka na mpinzani wake Abdullah Abdullah baada ya wawili hao kupinga matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini humo.
Duru zinaeleza kuwa, Serikali mpya ya Afghanistan itakuwa na jumla ya mawaziri 25 ambapo Rais Ashraf Ghani atateua 13 kati yao huku 12 wakiteuliwa na Abdullah Abdullah ambaye kwa sasa ndiye Afisa Mkuu Mtendaji wa Serikali (CEO). Mawaziri walioteuliwa watatakiwa kuidhinishwa na Bunge kabla ya kuanza rasmi kazi zao

No comments:
Post a Comment