Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya leo Ijumaa ameliongoza taifa kuadhimisha miaka 51 ya uhuru wa nchi yake.
Sherehe hizo zilizojaa mbwembwe zilifanyika katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo Marais Yoweri Museveni wa Uganda, John Dramani Mahama wa Ghana na Paul Kagame wa Rwanda. Viongozi wa muungano mkuu wa upinzani wa CORD nchini Kenya pia walihudhuria sherehe hizo.
Akizungumza kwenye hotuba yake, Rais Kenyatta amesema ugaidi ni tatizo la kimataifa na kusisitiza kuwa, vita dhidi ya ugaidi vinapaswa kuendeshwa kwa ushirikiano wa kila nchi duniani. Rais wa Kenya amewataka Wakenya kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto za kiusalama hususan ugaidi wa kundi la al-Shabab la Somalia. Kiongozi huyo amewaonya wale wanaoshirikiana na magaidi akisema chuma chao ki motoni. Amekanusha madai kwamba vita dhidi ya Ugaidi vinawalenga Waislamu na kusisitiza kuwa Waislamu ni wapenda amani na wanafaa wawakatae wanaojaribu kutumia dini yao kutenda vitendo vya kinyama dhidi ya Wakenya. Kundi la al-Shabab limekuwa likifanya mauaji ya kinyama dhidi ya raia wasio na hatia nchini Kenya kama njia ya kuishinikiza serikali ya Nairobi iondoe jeshi lake nchini Somalia.

No comments:
Post a Comment